Chokoraa, chokoraa
'talala wapi, 'taenda wapi
Chokoraa, chokoraa, ‘lilala wapi jana?
Mi sikulala poa! Chandalua kilinitekenya usiku mzima.
Chokoraa, chokoraa, ‘taenda wapi leo?
Mi n’taenda shule! Elimu muhimu, k’kuwa mzima bora.
Chokoraa, chokoraa, ‘takula nini leo?
Nimeshiba maziwa, mkate na maharagwe, ugali na msukumo wa wiki.
Chokoraa, chokoraa, je nguo ulizitoa wapi?
Yaani hujui, mbawa nzuri alama ya ‘dege mwema.
Na njumu je chokoraa, kwa nini miguu tupu tupu?
Mama angekuona, ’ngeadhibishwa na pati pati.
Chokoraa, chokoraa, kwa n’ni wavuta glue?
Niliambiwa kuvuta guluu, ‘tabongabonga ‘bongo.
Chokoraa, chokoraa, si uwache kuombaomba.
Si kizuri chokoraa, si kizuri, usikifanye.
Chokoraa, chokoraa, waniambia ‘ko na njaa.
Kwanini dada’ko kanukika samaki?
‘si chokore pipa chokoraa, pipa ya matupo, si’ ya mavuno.
Ndio sababu ‘menyesika, kazidia urafiki wa nzi.
Chokoraa, chokoraa, haumfahamu Mwenyezi Mungu?
Ndio maana bado kutopata, mabaraka wala sudi.
Chokoraa chokoraa, kashike Bibilia.
Omba kila siku! ‘subuhi, mchana, na usiku.
N’takuombea chokoraa, ili usaidike.
Baba aweza nisiyoyaweza, na Baba mwenyezi ‘takusaidia.
Chokoraa, chokoraa, ‘mesikia habari?
Mheshimiwa kasema, kila tafanikiwa.
Raisii kasema, chokoraa chokoraa,
chokora itainuliwa, chokoraa watainuliwa.
Chokoraa, chokoraa, ingawa ‘tatizo mengi,
hakuna kilicho kitamu, kuliko kile kilichopatikana kwa shida.
Kila la heri chokoraa, uwe na siku njema.
N’natarajia chokoraa, mabadiliko yanawasili.
Chokoraa, chokoraa, ‘talala wapi leo?
Chokoraa, chokoraa, ‘taishi vipi leo?
Chokoraa, chokoraa, ‘takula nini leo?
Chokoraa, chokoraa, ‘taomba nani leo?
‘sisahau chokoraa, ‘kaahidiwa,
kwamba nyinyi chokoraa, ham’tasahaulika.
Chokoraa, chokoraa, kikafa barabarani,
katupwa pipani, na kasahaulika milele.
K. Nzumbi Mutemi, 2026