Jina langu
Je Mama, jina langu litoka wapi?
Mimi
Je Mama, niliwa na swali,
nililolipenda kukuuliza.
Si swali gumu, wala swali zito,
lakini swali la muhimu.
Je Mama,
swali ambalo linalonichokoza ni hili,
jina langu, limetoka wapi?
Jina la pili, na la tatu,
Nzumbi na Mutemi,
ni sharti la kabila langu.
Swali nililonalo,
si kuhusu haya majina,
lakini jina langu la kiKristu.
Mama
Naam mwanangu, basi jiketize,
nikuelezee hadithi ya jina lako.
Na kweli,
si swali gumu, wala swali zito,
lakini jina,
la toto ni muhimu.
Ulipo tumboni,
bado kutoka,
Baba na Mimi tukakaa.
“Ni jina gani, tutammpa,
muwana muwetu,
kwani jina la toto ni muhimu.”
“Mpenzi wangu, shika kalamu,
aandika kisirisiri,
majina matano, yanayokupendeza.
Nami nitafanya kama wewe,
kuandika kisirisiri,
majina matano, yanayonipendeza.”
Kwa hamu na ghamu,
sote tukaandika kisirisiri,
majina yaliyotupendeza.
Tulipofananisha majina,
la kwanza, La!
la pili pia La!
La tatu, likawa sawa.
Baba aliandika Musa,
Nami niliandika Mustafa.
La kwanza, La! Hapana.
Baba aliandika Juma,
Nami niliandika Pascal.
La pili pia, La! Hapana.
Baba kaandika Kevin,
Nami kaandika Kevin.
La tatu, Lo! Yako sawa.
Baba kaandika Kevin,
Nami kaandika Kevin.
Lo!
La tatu, likawa sawa.
Mimi
Mama alitabasamu, nami nikatabasamu,
Jina la kwanza lililonifaa.
Bado ninatabasamu, bado anatabasamu,
“Je mwanangu, nimejibu swali uliyo?"
Mama umelijibu,
swali lisilo gumu,
zito, au dogo.
Lakini swali hilo,
lilo swali la muhimu,
je, jina langu litoka wapi?”
Kisha nakuuliza,
wewe mwenye jina,
jina lako limetoka wapi?
Si swali gumu,
au zito,
wala dogo au kubwa,
lakini swali la muhimu.
K. Nzumbi Mutemi, 2026